Mwigizaji Staa Kajala Masanja amefunguka kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu yanayoendelea mitandaoni kumuhusu yeye na EX wake Harmonize ambapo amekiri kwamba ni kweli miezi miwili kabla hajaachana na Harmonize alikuwa akichukua 10% kutoka kwenye kila hela aliyokuwa akiingiza Harmonize.
Akiongea leo Jijini Dar es salaam wakati akipewa dili la Ubalozi wa Pedi, Kajala pia amethibitisha madai ya Harmonize kumpa msaada Baba yake Mzazi ambapo amesema ni kweli lakini amekanusha madai kwamba ameuza Range aliyopewa na Harmo.
Kuhusu password za Benki za akaunti za Harmonize amesema sio yeye tu Vijana wote wa Konde Gang wanazo na kuhusu ishu ya Anjela kuondoka Konde Gang amesema hata yeye ameshangaa kwani aliwahi kumfuata Harmonize na kumuomba amuachie hata gari kwani ni Mgonjwa…full video ipo Youtube ya millardayo