Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Abdurahman Kinana wamemtakaka Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi, Bw. Saed Kubenea kuomba radhi kwa taarifa dhidi yao iliyochapishwa na gazeti la Mwanahalisi Tarehe 20 wezi July 2023 ikidai kwamba viongozi hao wanalipa fedha watu wanaopinga mkataba wa uwekezaji kati ya Serikali na kampuni ya DP world ya Dubai.
Katika barua hiyo ambayo imeandikwa kupitia kwa wakili Eric S. Ng’maryo Advocates, viongozi hao wamewasilisha madai yao kwa Bw. Kubenea wakimtaka kufuta kashfa hiyo na kuomba radhi ndani ya siku 14, la sivyo watachukua hatua za kisheria.
Barua hii ya madai imeeleza kiini cha kashfa hiyo ni tuhuma za uongo kwamba viongozi hawa wanachochea wale wanaopinga maendelezo ya bandari kwa kuwalipa fedha watu ambao hawajatajwa ili watu hao wapinge au waendelee kupinga maendelelezo ya bandari.
Kwa taarifa zaidi unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi na zaidi.