Mvutano umeongezea tangu siku ya Jumatano kati ya mamlaka ya kijeshi nchini Niger na Ufaransa, siku moja kabla ya mkutano muhimu wa ECOWAS.
Utawala wa kijeshi nchini Niger umeishutumu Ufaransa kwa kukiuka anga ya Niger na kuwaachia huru magaidi. hata hivyo Paris imekanusha madai hayo ikisema hayana msingi wowote.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Baraza la Ulinzi wa Taifa (CNSP), linaishutumu Ufaransa kwa “kupanga kuhatarisha usalama” kwa lengo la “kudhoofisha CNSP na kuchochea mgawanyiko na raia wa Niger”.
Viongozi wa mapinduzi nchini Niger wanatoa mfano wa “wafungwa 16 wa kigaidi walioachiliwa kwa upande mmoja na Ufaransa”. Kulingana na utawala wa kijeshi, kisha walikutana kuandaa mashambulizi katika eneo la mipaka mitatu.
Viongozi wa mapinduzi pia wanaishutumu Ufaransa kwa kukiuka anga yake ambayo ilifungwa siku ya Jumapili.
Ndege ya jeshi la Ufaransa A-400M iliondoka muda mfupi baada ya saa kumi na mbili Jumatano asubuhi, saa za Niger kutoka Ndjamena.
Kulingana na utawala wa kijeshi, mara tu ilipoingia kwenye anga ya Niger bila idhni, ndege hiyo ilikata mawasiliano yote kwa zaidi ya saa nne.
Tazama pia…..