Rais wa Tanzania Dkt. Samia akiwa kwenye maonesho ya Nanenane juzi alikata utepe na kuzindua ugawaji wa vifaa vya kutengenezea vihenge vya chuma kwa Vijana kqa ajili ya kuhifadhia mazao kama karanga na mahindi ili kuondokana na sumukuvu.
Clepin B. Josephat ambaye ni Project Coordinator wa mradi wa kudhibiti Sumukuvu nchini ( TANIPAC) amesema kuwa watajenga maghala 14 ambayo yatatumika kuhifadhia mahindi kwa lengo la kuondoa tatizo la sumukuvu kwenye mazao ya nafaka na mafuta pamoja na kuunganisha na kituo cha Mtanana.
Amesema baada ya ujenzi huo wanunuzi watanunua mazao katika soko hilo badala ya kwenda kununua mazao kwa mkulima.
Sumukuvu inaathiri zaidi mazao ya mahindi na karanga kutokana na namna ya na wakati wa kuvuna na kuhifadhi ambapo unyevuunyevu unaopatikana kwenye mazao husababisha uotaji wa fangasi na kuwa chanzo cha sumukuvu.
Mradi wa TANIPAC unalenga utakapo kamilika kuwezesha jamii kutumia njia sahihi na za kisasa za uhifadhi wa nafaka hususani mahindi kutokana na sumukuvu.
“Tatizo la sumukuvu linasababisha mazao ya wakulima kukosa bei nzuri kwenye masoko, hii hupelekea mkulima kupata hasara”