Tory Lanez anaanza kuhisi uzito wa kifungo chake cha miaka 10 jela baada ya kuamini kuwa kesi hiyo ingekwisha vyema kwake,lakini la hivyo sasa amgeukia Mungu.
Wakili wa Tory, Jose Baez, anaiambia TMZ mteja wake anahisi huzuni hivi sasa baada ya kutupwa jela.
Inasemekana kuwa Tory ana wakati mgumu kushughulikia hukumu hiyo, alimweleza wazi wakili wake kuwa ataendelea kuwa na nguvu na kukabiliana na muda wake wa kukaa jela kadri awezavyo.
Jose anasema Tory anategemea imani yake kwa Mungu, uungwaji mkono wa marafiki/familia yake na pole inayotolewa na wafuasi wake kote ulimwenguni — ambao wengi wao wanaomboleza kwa sauti kubwa kutokana na adhabu hiyo .
Rapa kutoka Canada Tory Lanez amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela, zaidi ya miezi saba baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga risasi msanii mwenzake wa muziki Megan Thee Stallion na kumjeruhi miguu baada ya tafrija ya pool huko Hollywood Hills Julai 2020.
Jaji wa Mahakama ya Juu ya Los Angeles, David Herriford, alitoa hukumu hiyo Jumanne kwa Lanez mwenye umri wa miaka 31, ambaye alipatikana na hatia kwa makosa matatu: kushambulia kwa kutumia bunduki ya kivita, kuwa na bunduki iliyojaa, ambayo haijasajiliwa kwenye gari na kufyatua silaha mbaya ikitajwa kama uzembe.