Kulingana na jarida la Ufaransa L’Equipe, klabu ya Saudi Pro League, Al Ahli imewasilisha ofa ya €12m kwa Liverpool ikiwa na matumaini ya kumsajili Thiago Alcantara msimu huu wa joto .
Mhispania huyo amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake huko Anfield na ndiye kiungo mkongwe zaidi katika klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 32. Alexis Mac Allister angerithi taji hilo akiwa na umri wa miaka 24 iwapo Thiago ataondoka.
Lakini kwa kupoteza mchezaji mwingine wa kiwango cha juu siku chache kutoka kwenye ufunguzi wa msimu kunaweza kuwa pigo kubwa kwa Klopp.
Kocha wa Liverpool Klopp amesikitishwa na nguvu za vilabu vya Saudia na hivi majuzi alitoa wito kwa FIFA kuchukua hatua juu ya dirisha lao la uhamisho linalofungwa wiki tatu baada ya tarehe ya mwisho ya Uropa.
Dirisha la usajili litafungwa katika ligi tano bora za Ulaya mnamo Septemba 1.
Vilabu nchini Saudi Arabia vina hadi Septemba 20 kukamilisha biashara zao, tayari zimewekeza pesa nyingi msimu huu wa joto.
Tofauti ya tarehe za mwisho inaweza kusababisha kuvurugika kwa vikosi barani Ulaya, iwapo Saudi Pro League itavutia wachezaji wengine wakubwa, kama vile Thiago.