Habari ya Asubuhi na Karibu kwenye matangazo yetu hii leo Ijumaa 11.8.2023
Urusi imezindua leo Ijumaa uchunguzi wake wa kwanza Mwezini baada ya miaka 50, ujumbe ulionuiwa kutoa msukumo mpya kwa sekta yake ya anga ya juu, ambayo imekuwa ikijitahidi kwa miaka mingi na kutengwa kutokana na mzozo nchini Ukraine.
Uzinduzi wa uchunguzi wa Luna-25 ni misheni ya kwanza mwezini kwa Moscow tangu 1976, wakati USSR ( Umoja wa zamani wa Sovieti) ilikuwa mwanzilishi katika suala la anga ya juu. Mpango ambao ulisitishwa kutokana na matatizo ya ufadhili na kashfa za ufisadi.
Roketi ya Soyuz iliruka kwa muda uliopangwa saa 02:10 saa za Moscow kutoka eneo la Vostotchny Cosmodrome katika Mashariki ya Mbali, kulingana na picha zinazotangazwa moja kwa moja na shirika la anga za mbali la Urusi, Roscosmos.
Chombo hicho kilipanda katikati ya moshi mwingi na moto chini ya anga ya kijivu. Kitafikia mzunguko wa mwezi katika siku tano, ambapo itatumia kati ya siku tatu hadi saba kuchagua mahali pazuri kabla ya kutua kwenye eneo la ncha ya kusini ya mwandamo.
Kulingana na chanzo ndani ya shirika la anga za mali la Urusi, Roscosmos, kilichohojiwa na shorikala habari la AFP, shirika hilo linapanga kutua kwa uchunguzi Agosti 21.
“Kwa mara ya kwanza katika historia, kutua mwezini kutafanyika kwenye ncha ya kusini ya mwezi. Hadi sasa, kila mtu alikuwa akitua katika eneo la ikweta”, amekaribisha afisa mkuu wa Roscosmos, Alexandre Blokhine, katika mahojiano ya hivi karibuni na Gazeti la Rossiïskaïa Gazeta.
Tazama Pia…..