Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane anatazamiwa kufanyiwa vipimo vya matibabu katika klabu ya Bayern Munich baada ya kupewa ruhusa ya kwenda Ujerumani na Tottenham.
Bayern na Spurs walikubaliana dili la thamani ya zaidi ya euro 100m (£86.4m) kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 siku ya Alhamisi.Uamuzi wa kuhama uliachwa kwa Kane, ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Tottenham akiwa na mabao 280 katika mechi 435.
Kane alikuwa amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake na hakukuwa na uwezekano wa kusalia na klabu hiyo.
Iwapo hakuna masuala yanayomzuia, uhamisho wa Kane utakamilika kwa wakati ili kuanza msimu wa Bundesliga wiki ijayo.I
lihisiwa mshambuliaji huyo alitaka uamuzi kuhusu mustakabali wake ufanywe kabla ya msimu kuanza, lakini imewachukua Bayern muda mwingi kufikia hatua ambayo mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy alikuwa tayari kufanya makubaliano.