Wafungwa katika gereza la Bahrain wameanzisha mgomo wa kula kutokana na hali mbaya ya magereza, ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa saa 23 na vizuizi vya maombi, jamaa na viongozi …walisema Alhamisi.
Jumuiya ya al-Wefaq ya Bahrain imetangaza leo Ijumaa kwamba mamia ya wafungwa wa Bahrain wamegoma kula wakilamikia hali ngumu ya magereza ikiwa ni pamoja na kuwekwa ndani ya seli kwa muda wa saa 23 kwa siku na kuzuiwa kufanya shughuli za kidini.
Mwanaharakati wa masua la sheria wa Bahrain, Ebtisam Al-Sayegh ametangaza kwamba idadi ya wafungwa wa kisiasa nchini Bahrain hivi sasa inazidi watu elfu mbili ambao wanaishi katika mazingira magumu sana.
Al-Sayegh amesema, inasikitisha kwamba, hali za wafungwa pia ni mbaya na zinazoandamana na ukatili. Amesema wafungwa hao wananyimwa haki za msingi kabisa, utu wao unadhalilishwa, wanaishi katika mateso ya kiakili na kimwili, na baadhi yao wanakufa taratibu kutokana na maradhi na kukosa huduma ya matibabu.
Bahrain ni mshirika mkuu wa kikanda wa Marekani na ni nyumbani kwa Meli ya Tano ya Jeshi la Wanamaji la Marekani.
Imewaweka jela wapinzani wengi tangu mwaka 2011, wakati mamlaka zinazoungwa mkono na jeshi la Saudia zilipokandamiza maandamano yaliyoongozwa na Washia kudai utawala wa kikatiba na waziri mkuu aliyechaguliwa.