Mwanamume mmoja, Hassan Umar, amefikishwa mbele ya mahakama ya hakimu mkazi mjini Kano, Jimbo la Kano, kwa madai ya kumuacha mpenzi wake baada ya mwanamke huyo kumtumia kiasi cha fedha cha Sh900,000 sawa na zaidi ta Tsh million 2.
Wakili wa mlalamishi aliambia mahakama kuwa mshtakiwa alidai alikuwa alipendana na mteja wake kwa makubaliano kwamba wangefunga ndoa lakini alimdanganya.
Alisema baada ya mteja wake kumtumia pesa, mshtakiwa alikataa kumuoa na badala yake alimuacha na kuacha kufika kwake kabisa.
Aliposomewa mashtaka hayo, mshtakiwa alikana.
Hakimu Mfawidhi, Salisu Hussaini, alizitaka pande zote mbili kuleta mashahidi wao katika kikao kijacho kilichoahirishwa.
Akizungumza baada ya kikao cha mahakama, mwanamke huyo alisema, “nina shaka hakunivutia, chochote alichoniuliza nilikifanya papo hapo.
Nilimpikia vyakula vya aina tofauti tofauti vikiwemo kuku, nyama na hata kondoo wawili na kumpatia zaidi ya Sh900,000 juu yake. Lakini kutoka hapo, alianza kunionyesha kana kwamba hakujali. Baadaye aliacha kuja kwangu.”