Serikali kupitia wizara ya mifugo na uvuvi na wizara ya Uchumi wa bluu Zanzibar imesema wataanza kutumia teknolojia mbali mbali kwenye vyombo vya uvuvi ikiwemo ufungaji wa camera mahususi kwenye vyombo hivyo zitakazosaidia katika kuangalia na kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa wavuvi wanaovua kwa njia zisizokuwa sahihi.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na naibu katibu mkuu wizara ya uchumi wa bluu Zanzibar Bw.Hamis Shibu ambapo amesema umuhimu wa kutumia teknolojia utasaidia kupambana na uvuvi haramu.
Kwa upande wake meneja wa hifadhi za bahari na maeneo tengefu Tanzania ambaye pia amewakilisha wizara ya mifugo na uvuvi Bi Immaculate Swale amesema ,mifumo hiyo inategemea kuanza julai mwakani huku kwa sasa watashiriki katika utoaji wa elimu juu ya matumizi ya mfumo huo.