Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC) Mkoa wa Iringa Salim Abri Asas amesema chama hicho mkoa wa Iringa kimeweka mkakati maalumu kuhakikisha ya kwama kunakuwepo na ofisi za CCM kila kata jambo amesema litasaidia kufanikisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kisiasa.
Amesema hayo leo tarehe 12 Agosti 2023 katika Mkutano Maalumu wa Mafunzo kwa wajumbe wapatao 700 wa Halmashauri Kuu zote za CCM za wilaya na mkoa mkoani Iringa.
Katiba Mkutano huo mgeni rasmi alikuwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Idara ya Oganaizesheni, Issa Haji Gavu.