Neymar anafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kukamilisha uhamisho wa kwenda katika klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia.
Klabu hiyo ililipa dau lililovunja rekodi la dunia la £200m kwa uhamisho wa Neymar kutoka Barcelona mwaka 2017.
Habari za kukaribia kuondoka kwa Neymar zinakuja chini ya saa 24 baada ya klabu hiyo kuthibitisha kuwa mshambuliaji Kylian Mbappe amerejeshwa kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza.
Al Hilal pia wamejaribu kuwanunua nyota wenzake wa Neymar PSG Lionel Messi na Kylian Mbappe msimu huu wa joto.
Hata hivyo, fowadi wa Argentina Messi aliamua kujiunga na Inter Milan huku Mfaransa Mbappe akitarajiwa kusalia PSG licha ya mvutano kuhusu kandarasi yake.
Klabu hiyo ya Saudia ilitoa pauni milioni 258 kwa Mbappe mwezi Julai lakini alikataa uhamisho huo wa mwaka mmoja.
Neymar ndiye mchezaji wa hivi punde zaidi wa hadhi ya juu kuhamia Saudi Arabia msimu huu wa joto baada ya Jordan Henderson, Ruben Neves na Roberto Firmino wote kukubaliana mikataba.