Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki amesema Serikali imedhamiria kuongeza ufanisi na kuboresha elimu nchini kwa kuhakikisha inanunua vitendea kazi kwa Maafisa Elimu wa Shule za Sekondari nchini kwa lengo la kuongeza usimamizi na ufuatiliaji, ufundishaji na ujifunzaji Shuleni.
Ameyasema hayo leo August 14, 2023 kwenye hafla ya ugawaji wa magari kwa Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri nane na Makao Makuu ya Wizara magari mawili iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Azania Jijini Dar es Salaam.
Amesema vitendea kazi yakiwemo magari yatasaidia kuongeza ufanisi na kuwawezesha Maafisa hao kutekeleza majukumu yao ya kutembelea na kukagua Shule, kufuatilia Walimu na kusikiliza changamoto badala ya kusubiri wafuatwe ofisini.
”Tunaamini kwamba hakutakuwa na visingizio kwa ninyi kutembelea na kukagua Shule, sasa mtaweza kuwafuata Walimu na kusikiliza changamoto zao hukohuko Shuleni kwao badala ya kuwasubiri wawafuate ofisini.”