Katika Uhamasishaji wa michezo kwa Vijana nchini, Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali wa Sekta hiyo husasani katika ngazi za Wilaya na Mikoa.
Siku ya Jumamosi kulifanyika Fainali za mchezo wa Rede Tanzania ambapo kulihusisha Timu kutoka Kinondoni na Timu kutoka Mbagala ambapo mshindi alifanikiwa kuondoka na kiasi cha Shilingi Milioni 3 huku Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni Shawiji Abdallah akiwa ni mgeni rasmi katika mashindano hayo.
Itakumbukwa Licha ya michezo kuwa ni sehemu ya burudani lakini pia imekuwa ni miongoni mwa sekta zinazotengeneza ajira kwa vijana wengi sana na kuwakwamua na changamoto ya Ukosefu wa ajira.