Tottenham wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Arsenal Folarin Balogun, kwa mujibu wa jarida la Italia La Gazzetta dello Sport.
Spurs wanawinda straika baada ya kumuuza nahodha wa Uingereza Harry Kane kwenda Bayern Munich kwa dau la awali la €100million (£86.2m).
Inadaiwa Tottenham wanavutiwa na Balogun.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Marekani, mwenye umri wa miaka 22, kwa sasa yuko nyuma ya Kai Havertz, Eddie Nketiah, Leandro Trossard na Gabriel Jesus katika kikosi cha kwanza huko Emirates (ingawa huyu anauguza jeraha la goti).
Arsenal wanaripotiwa kutaka €55m (£47.4m) kwa Balogun, ambaye alifunga mabao 22 wakati wa mkopo akiwa na Reims msimu uliopita.
The Gunners wanasita kumruhusu kuondoka tena kwa mkopo kwa sababu amebakiza miaka miwili tu kwenye mkataba wake uliopo.
Huenda sasa ni wakati mzuri zaidi kwa Arsenal kumuuza Balogun ikiwa wanataka kumnunua mshambuliaji huyo mahiri, lakini haijafahamika kama watakuwa tayari kumuuza kwa wapinzani wao wakali.
Balogun hakuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 20 cha Arsenal kwenye mchezo wa Forest.