Yule trafiki wakike wa Kenya ambae kwa sasa Wakenya wengi wanamuita Koplo Linda Okelo ameingia tena kwenye headlines huko huko Kenya na kwa sasa ameamua kwenda mahakamani kupinga hatua ya kamati ya kinidhamu iliyowekwa.
Hatua hiyo ni ya kuchunguza madai ya kuvaa sketi fupi ambayo imesemwa kuwa ilikua nje ya maadili ya kazi na sheria za Jeshi hilo la Polisi la nchini Kenya.
Kupitia kwa wakili wake Tom ojienda Koplo Lindah amesema kwamba hakufanya kosa lolote kuvaa sketi hiyo hadi kulazimika kuundwa kamati ya kumchunguza na kutoa maelekezo ya adhabu anayostahili.
Lindah amesema kwamba asubuhi ya April 26 alifanya mkutana na OCPD wa kituo cha kiambu ili kuelekezwa,ingawa mkuu huyo wa polisi hakusema lolote kuhusiana na mavazi aliyovaa.
Ingawa May 2 Lindah alichukuliwa hatua za kinidhamukwa kosa la kuvaa mavazi yaliyombana kulingana na sheria za huduma za polisi-alivyo kuwa amevalia sketi fupi iliyombana saa saba mchana nje ya tawi la benki ya KCB lililopo kiambu.
Linda amedai kwamba sketi iliyo zua utata alikabidhiwa na afisa anaye shughulika na sare za polisi mwaka 2003 na amekua akivaa kila siku na mabosi wake hawakuwahi kulalamika kabla ya tarehe 26 Aprili.
Wakili wake Ojienda amesema kwamba wakati wa kikao cha kamati hiyo may 7 na may 9 Bii Okelo alichukuliwa hatua kimakosa kwani hakukua na sababu za kumuhukumu kulingana na mavazi yake,kesi yake itatajwa june 12 mwaka huu.