Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewaalika wadau wote wa Sekta ya Kilimo nchini kushiriki kongamano la kimataifa la mifumo ya Chakula barani Afrika ambalo kwa mwaka huu linafanyika Jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo litawaleta pamoja wadau zaidi ya 3000 ambapo kutakuwa na wawasilisha maada 350 kutoka nchi zaidi ya 70 kote ulimwenguni.
Mkutano mkubwa wa mifumo ya Chakula Afrika 2023(Africa’s Food Systems Forum 2023 Summit) utafanyika kuanzia tarehe 4-8 September 2023 jijini Dar es Salaam.
Mkutano huu utawakutanisha zaidi ya washiriki 3000 kutoka nchi mbalimbali duniani, ikiwa ni pamoja na Wakuu wa nchi, Watu Mashuhuri, Wafanyabiashara, Wawekezaji na wataalam wa mifumo ya chakula.
Mkutano huu ni fursa kubwa kwa watanzania na taifa kwa ujumla, ikiwa ni wakulima, wafanyabiashara, wawekezaji na wadau wote wa kwenye mifumo ya chakula nchini.
Ili kushiriki mkutano huu, tembelea www.agrf.org kujisajili.