Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mheshimiwa Kenani Kihongosi amebaini uwepo wa Malipo hewa katika chama cha Ushirika cha uamsho aagiza Takukuru kuchunguza.
Pia amemweleza Afisa Ushirika kujitathimin na kujieleza kwa maandishi kwanini hayo yanatokea na yeye yupo.
Pamoja na hayo amesisitiza kuwa serikali haitanyamaza kwa wale wote wanaojaribu kucheza na fedha za wakulima wa Tumbaku katika Wilaya ya Urambo.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya yupo katika ziara ya kutembelea vyama vya Ushirika kubaini changamoto na kuhimiza kilimo cha tumbaku kwa wakulima.