Kwa mujibu wa taarifa hiyo maofisa wengine 20 wa jeshi walijeruhiwa kwenye shambulio hilo, sita kati yao wakijeruhiwa vibaya.
Taarifa ya wizara hiyo ya ulinzi imesema maofisa wake waliojeruhiwa katika shambulio hilo wamehamishiwa katika jiji kuu la Niamey.
Jeshi limesema zaidi ya watu wenye silaha mia moja waliokuwa wakitumia usafiri wa pikipiki waliuawa.
Ukanda wa Sahel umekuwa ukikabiliwa na changamoto ya makundi ya watu wenye silaha kwa zaidi ya muongo moja sasa.
Changamoto ya kiusalama inayoendelezwa na makundi ya watu wenye silaha iliaanzia kaskazini mwa nchi ya Mali mwaka wa 2012 kabla ya kusambaa katika nchi jirani za Niger na Burkina Faso mwaka wa 2015.
Makundi hayo yenye silaha yamekuwa yakitekeleza mashambulio na kutangaza kuwa na ushirikiano na wapiganaji wa Islamic State na wale wa Al-Qaeda.
Maeflu ya wanajeshi, maofisa wa polisi wameripotiwa kuawaua katika mashambulio hayo, mamilioni ya raia wakiwa wameyakimbia Makazi yao kwa hofu ya kushambuliwa.