Mwenyekiti wa Bodi, Salim Muhene ( @salim_tryagain ) amehudhuria kozi ya Diploma katika Uongozi wa Klabu inayotolewa na FIFA (Diploma in Club Management) inayofanyika Jijini Sydney, Australia ambapo amepata nafasi ya kukutana na kuzungumza na Rais wa FIFA, Gianni Infantino kuhusu Africa Super League na ushiriki wa Simba kwenye michuano hiyo lakini pia kuzungumzia mambo mengi yanayohusu maendeleo ya mpira wa miguu Baranni Afrika na hususani Tanzania.
Rais Infantino amepongeza hatua kubwa ya maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika na zaidi Tanzania lakoni pia ameipongeza Tanzania kwa kazi kubwa ambayo inafanyika katika kukuza mpira akifurahishwa zaidi Simba na vilabu vingine chini ya usimamizi mzuri wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).