Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inapanga kuandaa Mkutano wa kilele wa Biashara kati ya Afrika, China na Marekani wa mwaka 2024.
Hayo yamezungumzwa katika mkutano kati ya Katibu Mkuu wa EAC, Dk Peter Mathuki na Rais wa Jumuiya ya Wakurugenzi Watendaji wa Marekani wenye asili ya China, Bw Robert Sun.
Dk Mathuki alimkaribisha Bw Sun mjini Arusha Jumanne ili kujadiliana kuhusu fursa za uwekezaji katika nchi zote washirika wa EAC.
Viongozi hao wawili walijadili mipango ya EAC kuandaa Mkutano huo unaotarajiwa kuvutia zaidi ya Wakurugenzi na wawekezaji 500 kutoka China na Marekani, ambao wanatafuta fursa za uwekezaji katika EAC.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Peter Mathuki, pia alizungumzia juu ya urejeshaji wa amani Mashariki mwa DR Congo kuwa uko mbioni.
Aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa na matumaini kwamba pande zote zinazopigana katika mzozo wa miongo kadhaa zingepatana.
Alikanusha kuwa Jeshi la Kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF) ambalo lilitumwa katika eneo lenye matatizo mwishoni mwa mwaka jana, limeshindwa kutekeleza majukumu yake.
“Hali si kama ilivyokuwa kabla ya askari kutumwa huko”, alisema, akibainisha kuwa alikuwa akitafuta kusitishwa kwa mapigano katika muda wa miezi michache.
Aliongeza kuwa EARCF ina uungwaji mkono na baraka za mataifa washirika katika umoja huo na isionekane kuwa ni nguvu isiyo halali.
“Dhamira yake ni kuhakikisha kuwa amani inarejeshwa nchini DRC”, alisema, akibainisha kuwa EAC imeweka mikakati miwili ya kisiasa na kijeshi ili kuhakikisha kuwa hali inarejea katika hali ya kawaida katika taifa hilo kubwa zaidi la EAC.
Tazama pia….