Neymar Jr. alikua mchezaji wa hivi punde katika safu ndefu ya wachezaji kuhamia Mashariki ya Kati alipojiunga na klabu ya Saudi Pro League Al Hilal kutoka kwa klabu ya Ufaransa ya Paris Saint-Germain, lakini supastaa huyo wa Brazil anamsifu mmoja wa wapinzani wake kwa kuanzisha ligi ya nchi hiyo.
‘Ninaamini Cristiano Ronaldo alianzisha haya yote na kila mtu alimwita kichaa,na hivi na vile leo, unaona ligi inakua zaidi na zaidi,fowadi huyo wa zamani wa PSG aliambia chaneli za kijamii za Al Hilal.
Ronaldo alisaini mkataba wa miaka miwili na nusu unaoripotiwa kuwa na thamani ya zaidi ya euro milioni 200 ($220.16 milioni) na Al-Nassr Desemba 2022 baada ya kuondoka Manchester United na tangu wakati huo, Karim Benzema, N’Golo Kanté, Kalidou Koulibaly, Edouard Mendy, Roberto Firmino, Sadio Mané na Marcelo Brozović wamekuwa miongoni mwa majina ya nyota waliohamia Saudi Pro League
‘Ninasukumwa na changamoto, alisema Neymar baada ya kuhama.
‘Ni wazi,unapokabiliwa na changamoto kama hii huongeza kustahimili kwako na nipo hapa kusaidia ligi
kukua zaidi na zaidi.