Wizara ya Elimu nchini Korea Kusini imeidhinisha sheria mpya itakayowapa walimu haki ya kumtia adabu mwanafunzi yeyote anayefanya utovu wa nidhamu, baada ya maandamano ya kupinga unyanyasaji wa wanafunzi na wazazi wao.
Kuanzia Septemba, walimu wana uwezo wa kuwafukuza wanafunzi wanaopiga kelele darasani wakati wa masomo na kuwanyang’anya simu zao wale waliokamatwa na simu darasani.
Sheria haiwaruhusu kumpiga mwanafunzi au kumpa nidhamu kali, bali walimu wana uhuru wa kutoka nje ya chumba cha mabishano kati ya wazazi wa wanafunzi na walimu iwapo wataanza kuwatolea maneno ya kashfa au matusi.
Haya yanajiri baada ya mwalimu mmoja kujiua mwezi Julai, kwasababu ya kunyanyaswa na wazazi wa baadhi ya wanafunzi ikiwa ni pamoja na kupigana alipokuwa akifundisha.
Hapo awali haikuwa halali kwa walimu kupiga wanafunzi nchini Korea Kusini au nchi nyingine yoyote kwani adhabu ya kimwili kwa wanafunzi kwa ujumla inachukuliwa kuwa njia isiyofaa na yenye madhara ya nidhamu.
Nchini Korea Kusini, Sheria ya Elimu ilikataza walimu kutumia adhabu ya kimwili au njia nyingine yoyote ya viboko kuwaadhibu wanafunzi hii ni pamoja na kupiga, kuchapa au aina nyingine yoyote ya nguvu ya kimwili na walimu wanaokiuka katazo hili waliweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu, ikiwa ni pamoja na kuachishwa kazi.