Mjumbe Wa Baraza la Kuu la Vijana Uvccm Sameer Murji eo Tarehe 18/07/2023 ametembelea shamba la Vijana na kuona Ofisi ya Chama cha Mapinduzi kata Ufukoni na kujionea nguvu kazi za Vijana katika shamba la kata ya Ufukoni Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Mjumbe wa Baraza Kuu uvccm Taifa CDE Sameer Murji baada ya kukagua eneo la shamba pamoja na Ofisi ya chama Cha Mapinduzi kata ya Ufukoni na amefanya Mkutano wa pamoja na Uongozi wa Vijana ulioshirikisha Viongozi mbalimbali wa Serikali na Viongozi wa Chama na Jumuiya zote katika kata ya Ufukoni na kufanya Matukio Kama Yafuatayo.
Ambapo katika Mkutuano huo amegawa Jezi seti mbili na Mipira Miwili kwa Team ya Wavulana ya kata na Team ya wanawake ya Kata na Pesa Taslim Laki 300,000/= Kwa lengo la kusaidia Shughuli za kuendeleza MRADI wa Vijana kata ya UFUKONI Kuunga Mkono Jitihada za Dkt, Samia Suluhu Hassan katika Muendelezo wa Program ya BBT.
1.Ufukoni boys
2.Ufukoni Queen.
Aidha Mjumbe CDE Sameer Murji amewaasa Vijana kujituma na kufanyakazi kwa bidiii, ili kuonesha juhudi zao katika kufanya Shughuli ili kuinua Uchumi hususani shughuli zinazotokana na Kilimo na miradi mbalimbali.
Sambamba na hilo Mjumbe wa Baraza Kuu uvccm Taifa amekabidhi Kadi ya Uanachama kwa kijana mmoja (1) baada Kijana kurudisha kadi ya CUF ameamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi na Kuunga Mkono Juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mama Dkt Samia Suluhu Hassan.