Ni Headlines za Wakali ama wauzaji wa Simu za Samsung kutokea Tanzania ambapo time hii imetangaza rasmi uwepo wa kizazi chake cha tano cha simu za Galaxy zinazofunguka (foldables): Galaxy Z Flip5 na Galaxy Z Fold5 katika soko la Tanzania.
Uzinduzi huo umefanyika Dar es Salaam ambapo uliwakutanisha wadau wakiwemo Mabalozi wake ambae ni Mchekeshaji Idris Sultan.
Mkuu wa Biashara wa Samsung Tanzania, Bwana Manish Jangra, alisema Galaxy Z Fold5 ni simu bora yenye kioo kikubwa inayotoa uzoefu wa kipekee.
“Fold ina kioo kikubwa na ni simu yenye uwezo inayotoa burudani ya utazamaji wa kuvutia, betri inayodumu kwa muda mrefu katika muonekano mwembamba na ikiwa nyepesi. Galaxy Z Fold5 ni rahisi kubeba popote, lakini ina utendaji wenye nguvu zaidi katika mfululizo wa Galaxy Z series. S Pen Fold Edition iliyotambulishwa kwenye kizazi cha tatu cha Fold mwaka 2021, imeboreshwa ili kutoa uzoefu bora wa kuandika kwenye Galaxy Z Fold5.
Huduma na vifaa hivi viinaungana ili kutoa ufanisi mkubwa kwenye kioo kubwa na kuruhusu watumiaji kukamilisha kazi muhimu popote watakapokuepo,” alisema.
“ZFold inatoa uzoefu kama wa kompyuta kibao inapofunguliwa. Kifaa hiki ni kamilifu kwa kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja, kwani kinakuruhusu kuendesha programu nyingi kwa wakati mmoja kwenye kioo kubwa, kutokana na huduma yake ya Multi-Active Window,” alielezea.
Kwa mujibu wa Bw. Jangra, Chini ya kifuniko, ZFold inaendeshwa na processor ya Snapdragon 865, ikiambatana na RAM ya 12GB, ikitoa kasi na utendaji usio na kifani. Kwa upande wa maisha ya betri, ZFold ina betri ya 4500mAh, inayohakikishia unaweza kuwa na ufanisi na ukipata burudani kwa muda wote wa siku. Vile vile, simu hii ina uwezo wa 5G, ikikuruhusu kupata kasi ya mtandao ya haraka popote uendapo.
Nae Mchekeshaji Idris Sultan alisema..’Kwanza nichukue nafasi hii ya kipekee tangu niwe balozi wa simu hizi za Samsung sijawahi kuwaangusha na ni simu imara na nzuri wakati wowote ule hususani wale wapenzi wa picha tunajua ama najua tutakuwa tunaongea lugha moja ni kali na ni nzuri kabisa, unyama ni mwingi wazee Galaxy Z Flip5 na Galaxy Z Fold5 unyama ni mwingi’