Hili ndilo swali linalotawala hadithi na vichwa vya habari kote kanda na kwa hakika ambalo limeacha taifa lisilo na bahari la Niger katika mchanganyiko wa hasira, woga na ukaidi usio na kifani.
Baada ya mikutano kadhaa ya wakuu wa ulinzi wa Afrika Magharibi, mkutano wa hivi punde zaidi uliofanyika mjini Accra, Ghana siku ya Alhamisi tarehe 17 Agosti, jibu la swali hili ikiwa wazi kabisa linabakia kuwa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) haiachi tishio la kuingilia kijeshi. Wanasisitiza kwamba chaguo la uingiliaji wa silaha bado liko kwenye meza.
Abdel-Fatau Musah, kamishna wa ECOWAS siku ya Alhamisi alisema nchi zote wanachama isipokuwa zile zilizo chini ya utawala wa kijeshi na Cape Verde zimekubali kuchangia wanajeshi kwa ajili ya kikosi hiki cha kusubiri.
Macho yote sasa yameelekezwa kuona hatua inayofuata baada ya kuwezesha kikosi cha kusubiri cha kambi ya kikanda. Operesheni zitaanza lini, wanajeshi wangekusanyika wapi na wanakusudiaje kuingia Niger ambayo mipaka yake kwa sasa imefungwa kwa Nigeria na Jamhuri ya Benin?
ECOWAS ilikuwa Julai 30, ilitangaza ukanda usio na ndege, kufungwa kwa mipaka na Niger, na kusimamishwa kwa miamala ya kibiashara na kifedha. Wamewataka viongozi wa mapinduzi nchini humo kumwachilia huru Rais Mohamed Bazoum baada ya kuondolewa madarakani Julai 26. Lakini mamlaka nchini Niger zikiongozwa na kiongozi wa mapinduzi Jenerali Abdourahamane Tiani bado zinapinga.
Kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya na viongozi wa mapinduzi wiki iliyopita kulionekana kuashiria kuanza kwa mpito kwa serikali mpya. Waziri Mkuu Ali Mahaman Lamine Zeine ana jukumu la kuongoza utawala huo wenye wanachama 21, huku majenerali kutoka baraza jipya la uongozi wa kijeshi wakiongoza wizara ya ulinzi na mambo ya ndani.
Siku ya Jumatano tarehe 16 Agosti, habari ziliibuka kwamba kundi la wenyeji wa Niamey, mji mkuu wa Niger wanalenga kuajiri makumi ya maelfu ya watu wa kujitolea kutoka nchini kote kujiandikisha kwa Wanajitolea kwa ajili ya Ulinzi wa Niger.