Kulingana na ripoti kutoka Uturuki, uongozi wa Chelsea umemjulisha Hakim Ziyech kwamba anaweza kuondoka kwenda Galatasaray kwa uhamisho wa bure.
Chelsea ilifikia makubaliano na klabu ya Saudia Al-Nassr mapema msimu huu wa joto kumuuza Ziyech kwa pauni milioni 8 lakini dili hilo liliporomoka baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco kufeli vipimo vyake vya afya.
Ziyech tangu wakati huo amejikuta katika hali ya sintofahamu huko Stamford Bridge kwa kuwa hayumo katika mipango ya Mauricio Pochettino.
Chelsea iko tayari kumuacha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 aondoke bure huku The Blues wakijaribu kuondoa mbao zilizosalia Stamford Bridge, na kupata hasara ya £33.3m kwenye uwekezaji wao wa awali walioufanya wakati wa kumsajili kutoka Ajax Februari 2020.