Thierry Henry anatarajiwa kuwa kocha mkuu mpya wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 baada ya kuchaguliwa na Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF), vyanzo vimeiambia ESPN.
Henry, ambaye aliacha nafasi yake kama msaidizi wa Ubelgiji baada ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar, atachukua mikoba ya Sylvain Rippoll kufuatia uchezaji mbaya wa Ufaransa kwenye michuano ya Euro msimu huu ambapo walitolewa na Ukraine katika hatua ya robo fainali.
Henry alishinda Kombe la Dunia na Euro katika siku zake za kucheza na pia alikuwa sehemu ya kikosi kilichofika fainali ya Kombe la Dunia 2006 ambapo walipoteza kwa Italia kwa mikwaju ya penalti.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 46 amekuwa na wakati mgumu katika muda wake mfupi wa ukocha kufuatia kutofanikiwa kuinoa Monaco na Montreal.
Kulingana na vyanzo, Henry alipunguzwa mshahara ili kuchukua nafasi mpya ya U21 na ana nia ya kuwaongoza kutwaa medali ya dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao huko Paris.