Shirikisho kuu la mchezo wa chess duniani limeamua kuwa wanawake waliobadili jinsia hawawezi kushindana katika hafla zake rasmi kwa wanawake hadi uhakiki wa hali hiyo utakapofanywa na maafisa wake.
Uamuzi huo wa Lausanne, shirikisho lenye makao yake makuu Uswizi Fide ulichapishwa siku ya Jumatatu na umekosolewa na makundi ya utetezi na wafuasi wa haki za watu waliobadili jinsia.
“Mabadiliko ya jinsia ni mabadiliko ambayo yana athari kubwa kwa hadhi ya mchezaji na kustahiki kwa siku zijazo kwa mashindano, kwa hivyo inaweza kufanywa tu ikiwa kuna uthibitisho unaofaa wa mabadiliko yaliyotolewa,” shirikisho hilo lilisema.
“Ikitokea kwamba jinsia ilibadilishwa kutoka kwa mwanamume hadi mwanamke mchezaji hana haki ya kushiriki katika hafla rasmi za Fide kwa wanawake hadi uamuzi zaidi wa Fide utakapofanywa,” ilisema.
Maneno ya uamuzi huo yanakuja wakati shirikisho hilo likiandaa hafla ya Kombe la Dunia huko Azerbaijan ambapo wachezaji wa juu akiwemo nambari 1 aliyeorodheshwa Magnus Carlsen wanahudhuria.
Shirikisho lina mashindano ya wazi ambayo inaruhusu wachezaji wote kushiriki, pamoja category maalum kwa wanawake, wachezaji wachanga na hata kompyuta.