Muuguzi wa Uingereza alipatikana na hatia Ijumaa ya kuwaua watoto saba wachanga na kujaribu kuwaua wengine sita katika kitengo cha watoto wachanga alichofanya kazi, na kuwa muuaji mkuu zaidi wa watoto nchini Uingereza.
Mahakama ya Manchester Crown Court kaskazini mwa Uingereza ilifikia maamuzi yake yote baada ya kujadiliana kwa siku 22.
Letby alikamatwa kufuatia msururu wa vifo vya watoto katika kitengo cha watoto wachanga cha Hospitali ya Countess ya Chester kaskazini magharibi mwa Uingereza kati ya Juni 2015 na Juni 2016.
“Lucy Leby alikabidhiwa kulinda baadhi ya watoto wachanga walio hatarini zaidi. Wale waliokuwa wakifanya kazi pamoja naye hawakujua kwamba kulikuwa na muuaji kati yao,” Mwendesha Mashtaka Mkuu Pascale Jones alisema katika taarifa.
“Mara kwa mara, aliwadhuru watoto wachanga, katika mazingira ambayo yangepaswa kuwa salama kwao na familia zao,” mwendesha mashtaka aliongeza, akiita mauaji hayo “usaliti kamili wa imani iliyowekwa ndani yake”.