Mjumbe Wa Baraza la Kuu la Vijana Uvccm Sameer Murji leo Tarehe 19/07/2023 aliongoza na Viongozi mbalimbali kata ya Mtwara Mjini kwenda kuwafarji Wanafunzi waathirika wa janga la Moto katika Shule ya Sekondari ya Kutwa Sabasaba.
Akizungumza na millardayo.com na alisema..’Nikiwa Kama Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Uvccm Taifa CDE SAMEER MURJI nimeongozana Pamoja Viongozi mbalimbali wa Vijana Baadhi ya kata ya MTWARA MJINI kwenda kuwafariji Wanafunzi waathirika wa Janga la Moto katika Shule ya Secondary ya kutwa Sabasaba kwakupoteza Vifaa vya kujisomea na nimeweza kujionea Jengo lililoathirika na Moto Siku JumatatuTarehe 14/07/2023 Pia Nimetoa Vifaa Vya kujisomea Kwa WANAFUNZI 31 kwakila Mmoja Nimempatia
1.Counter 5Pc
2.Peni. 4Pc
3.Ruler. 1pc
4.Mathematic table 1Pc
Nimewapatia pole kwa matatizo waliyoyapata Sambamba na hilo nimetoa nasaa kwa wanafunzi kuwa watumie muda wao kwa lengo la kuwa busy katika kujiandaaa na mitihani ya kumaliza Elimu yao ya Secondary’- Mjumbe Wa Baraza la Kuu la Vijana Uvccm Sameer Murji
‘Nimewataka Vijana kujituma kwa bidiii katika Vipindi vyao Vya Masomo wajisomee kwa Bidiii ,Wawe na Nidhamu kwa Walimu wao,Wamuombe Mwenyezi MUNGU kila Muda,Wapendane,Wasaidiane, Wanafunzi wawe na Utafiti Wa Kina Kwakila Jambo na Waishi Kwakumtegemea Mungu’-Mjumbe Wa Baraza la Kuu la Vijana Uvccm Sameer Murji
‘Nimetoa Salaam kutokea kwa Mama yetu Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa anawapenda Sana hata hivyo nimewaambia kuwa waendelee kumuombea Mema na mazuri Mama yetu kipenzi Chetu Dkt Samia Suluhu Hassan endelee kulitumikia Taifa letu Kwa Maslahi mapana ya Taifa na Ahadi ya Mama iko pale pale katika kuendeleza kutokomeza zero Mashuleni kwahiyo kila Mwanafunzi ana kila Sababu ya kufanya bidii katika masomo yake’- Mjumbe Wa Baraza la Kuu la Vijana Uvccm Sameer Murji