Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma Jijini Arusha leo August 19,2023 ambapo amewataka Watendaji watekeleze majukumu yao kwa ufanisi na wasimlazimishe kupanguapangua.
“Katika kuhakikisha Mashirika yetu yanajiendesha kwa tija na kupunguza gharama za uendeshaji kutoka Serikalini ni muhimu Ofisi ya Msajili wa Hazina isimamie sheria na kanuni zilizopo ikiwemo utekelezaji wa mikataba na utendaji kazi, tupate taarifa sahihi kwa wakati pale Vyombo vya Usimamizi wa Bodi na Mabaraza na Watendaji wakuu wakishindwa kutimiza vigezo mlivyokubaliana ili hatua stahiki zichukuliwe”
“Siku za karibuni nimewaapisha Wakuu wa Mashirika na nimewaambia nakukabidhi Shirika likifa kufa nalo na hilo sitanii Ma-CEO na Wenyeviti wa Bodi hatutanii, Serikali imeshatoa fedha nyingi hatuoni tija saa ni kuwekeana target za kuzalisha faida ambazo ukishindwa, kufa na Shirika lako”
“Kuna Mashirika hayachangii chochote Serikalini kutokana na hali ya Mashirika hayo, mageuzi tunayofanya ni lazima, ili Mashirika yajiendeshe na Serikali ipate msukumo”
“Wakati tulipolazimishwa kila Shirika litoe gawio, Ma-CEO na Bodi walikuwa kwenye wakati mgumu wanaamua kwenda kukopa watoe gawio, nikasema hapana wanaozalisha faida ndio watoe gawio sasa baada ya maboresho tunayokwenda kufanya kila CEO na Bodi zikajitafakari”
“Nataka kuona Taasisi zikichangia kutokana na kipato wanachozalisha kwa kutekeleza majukumu yao na sio kwenda kukopa ili kuchangia mfuko mkuu na hapa wale wanaohisi wataweza kwenda na safari hii basi wabadilike lakini wanaohisi kwamba mmh kwa haya mambo yanavyokwenda Mimi siwezi mlango wangu upo wazi njoo uninong’oneze Mama kwa haya mambo yanavyoweza nitafutie pengine huku siwezi”
“Kwahiyo tutapanguana tu na msiende kunilazimisha Mimi kupangua kwasababu sio jambo ninalolipenda, pangua pangua sio jambo ninalolipenda na mkiona nimepangua imenibidi kufanya hivyo”