Wakala wa barabara nchini-TANROADS imeanza kukagua mradi wa pili kati ya saba ya kuunganisha mitandao ya barabara kwa viwango vya lami nchini kwa utaratibu wa Usanifu, ununuzi na ujenzi kwa pamoja yaani EPC+F (Engineer, Procurement, Construction + Finance) ambayo ni dhana inayomuachia mkandarasi majukumu yote ya usanifu,ununuzi na Ujenzi.
Katika kuhakikisha na kuendana na kasi ya amamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuinua Uchumi wa watanzania nchini haswa katika maeneo yenye uchumi mfu ambao moja ya sababu ya kutokukua kwa uchumi katika maeneo husika ni kutokuwepo kwa miundombinu sahihi ya Barabara inayoweza kuunganisha maeneo hayo katika shughuli za kiuchumi.
Wakala wa barabara nchini TANROADS imeweza kuunganisha daraja la mto sibiti katika mradi huu ambao utaunganisha mikoa ya Simiyu, Singida, Manyara na Arusha ikiwa ni kiunganishi cha ukanda wa Magharibi, Kati na Kaskazini kwa barabara ya kiwango cha lami yenye kumla ya kilometa 339.
Daraja hili ni moja ya kiungo muhimu katika utekelezaji wa mradi huu mabao utarahisisha shughuli za kiuchumi kama Kilimo hasa mazao ya Mahindi, yitunguu Maji, Mbaazi, Vitunguu Saumu, Alizeti, Ngano na Nclizi.
Shughuli zingine za kiuchumi ni pamoja na Uvuvi, Ufugaji hasa Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo na Kuku, uchimbaji wa Madini (Endagemu) pamoja na Biashara ndogo ndogo kwenye maeneo ya Vijiji (Village Centers).
Meneja wa miradi ya Public Private Partinerships- PPP na Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC +F) Mhandisi Harold Kitainda amewaeleza Wananchi amabo wako katika maeneo ambayo mradi huo utapita kuwa miradi hii itaweza kuchangia kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.
“Mradi huu ni moja katinya mirada saba mikubwa ambayo Raisi wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amejikita kuitekeleza ili kuweza kuunganisha maeneo yote ambayo ni mazuri kiuchumi katika taifa letu ili maeneo haya yapitike ili yaweze kuchangia katika Uchumi wa Taifa”
Mategemeo ya Mradi huu kukamilika ni kuwa Wananchi wa Maeneo yote yanayopitiwa na Mradi huu wataweza kusafiri na kusafirisha Mazao yao kwa urahisi zaidi na kwa Muda mfupi na hivyo kujiongezea kipato na kuinua Uchumi wao na wa Taifa kwa Ujumla/ Vilevile ujenzi wa Barabara hii utapunguza gharama za uendeshaji kwa wamiliki wa Vyombo vya moto kama Magari na Pikipiki kwani utapunguza uaribifu wa Vifaa vya Magari na hivyo kuwezesha upatikanaji wa Vipuri kwa urahisi na kwa bei Nafuu.