Afrika Kusini haitalazimishwa kuunga mkono mamlaka yoyote ya kimataifa, Rais Cyril Ramaphosa alisema Jumapili alipokuwa akijiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa mataifa makubwa yanayoinukia kiuchumi.
Mkutano mjini Johannesburg wiki hii wa mataifa ya BRICS – Brazil, Russia, India, China, na Afrika Kusini – utatafuta kupanua ushawishi wao na kusukuma mabadiliko katika siasa za kijiografia duniani.
Uenyeji wa mkutano huo wa kilele wa Afrika Kusini umegeuka kuangazia uhusiano wake na Kremlin, haswa kwani imekataa kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
“Wakati baadhi ya wapinzani wetu wanapendelea kuungwa mkono waziwazi na uchaguzi wao wa kisiasa na kiitikadi, hatutaingizwa kwenye mchuano kati ya mataifa yenye nguvu duniani,” Ramaphosa alisema katika hotuba yake kwa njia ya televisheni ya Hali ya Taifa.
“Tumepinga shinikizo la kujilinganisha na mojawapo ya mataifa yenye nguvu au kambi zenye ushawishi wa mataifa,” alisema.
Ramaphosa atajumuika kwenye mkutano wa kilele wa BRICS na Rais Xi Jinping wa China, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da silva