Johannesburg inawapokea kuanzia Jumanne hii na hadi Alhamisi wakuu wa nchi za Brazil, China, India, na mkuu wa diplomasia ya Urusi, pamoja na viongozi wengine wa nchi za kusini, wakiwemo viongozi zaidi ya thelathini kutoka Afrika .
Rais Cyril Ramaphosa alihutubia taifa katika hotuba ya televisheni siku ya Jumapili ili kufafanua mkakati wa serikali yake katika masuala ya uhusiano wa kimataifa.
Rais wa Afrika Kusini alirejelea katika moja ya masuala makuu yatakayokuwa kwenye ajenda ya mkutano huu wa 15 wa Brics, yaani suala la upanuzi wa kundi hilo, na uwezekano wa kutoa nafasi kwa nchi nyingine: “Zaidi ya nchi ishirini kutoka kote dunia wametuma maombi rasmi ya kujiunga na BRICS.
Na Afrika Kusini inaunga mkono kuongeza wanachama.
Muungano wa Brics bado unatawaliwa na China, ambayo Cyril Ramaphosa anaifahamu vyema, kwa kuwa ziara ya rais Xi Jinping imepangwa Jumanne, wakati Beijing ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Pretoria: “Kuwa mwanachama wa BRICS kumeleta matumaini.
fursa kwa nchi yetu ya Afrika Kusini. Na hilo limewezesha uchumi wetu kuunda ushirikiano wa kimkakati na China, nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani. ”
Katika hatua ya kusawazisha, pia alitoa hoja ya kukumbusha, wakati wa hotuba hiyo, kwamba nchi yake itakuwa mwenyeji, mwezi wa Novemba, wa mkutano wa kilele wa AGOA kwa ushirikiano na Washington, pamoja na mkutano kati ya Afrika Kusini na Umoja wa Ulaya mwishoni mwa mwaka.
#RFI