Kenya na inalenga kuimarisha uhusiano wake na nchi ya Indonesia ilikuinua viwango vya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.
Katika kikao kati ya rais wa Kenya William Ruto na mgeni wake rais wa Joko Widodo, rais Ruto mataifa hayo mawili pia yalenga kujiendeleza katika sekta ya uwekezaji.
Uwekezaji kati ya nchi hizo mbili katika kipindi cha mwaka uliopita, ulikadiriwa kuzalisha zaidi ya dolla milioni mia sita.
Kwa mujibu wa hotuba ya rais Ruto, nchi hizo aidha zinatoa kipau mbele katika sekta za nishati, madini na uzalishaji wa mafuta.
Kenya pia inalenga kupata uungwaji mkono kutoka kwa nchi ya Indonesia kuisaidia kuingia katika masoko ya nchi za kusini mashariki mwa nchi za Asia, eneo ambalo uchumi wake unakuwa kwa kasi katika ukanda wa bara Asia.
Kwa upande wake rais Widodo amesema nchi yake itafanya kazi na Kenya kuendeleza ukuwaji wa mataifa hayo mawili.
Kiongozi huyo pia amesisitiza kuwa nchi yake inalenga kuhakikisha kwamba ushirikiano kati yake na Kenya unaleta faida kwa raia wa nchi husika.