City wanatafuta mshambuliaji mwingine baada ya kumuuza Riyad Mahrez kwa Al Ahli ya Saudi Arabia kwa £30m na Doku ameibuka kuwa mshindani mkuu kuchukua nafasi ya Mualgeria huyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ni mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji na amekuwa akihusishwa na timu kadhaa za Ligi Kuu msimu huu wa joto.
Ombi la West Ham lilikataliwa na Rennes kwaajili ya Doku mapema mwezi huu huku wagonga nyundo hao wasiweze kumnunua tena kufuatia nia ya City.
Doku tayari amefunga katika mechi zake mbili za kwanza akiwa na Rennes msimu huu na kufunga sita msimu uliopita kwenye Ligue 1.
Doku anaweza kuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na City majira ya kiangazi baada ya kuwasili kwa Josko Gvardiol na Mateo Kovacic, huku wawili hao wa Croatia wakigharimu pauni milioni 107.6 kwa pamoja.
Mpaka sasa wapo kwenye mazungumzo na Rennes kumsajili winga wa Ubelgiji Jeremy Doku na inadhaniwa kuwa angekuwa mbadala wa Riyad Mahrez, ambaye amehamia Saudi Arabia