Muuguzi Lucy Letby alipatikana na hatia ya kuwaua watoto saba katika kitengo cha watoto wachanga katika Hospitali ya Countess ya Chester kati ya Juni 2015 na Juni 2016 pia alipatikana na hatia ya kujaribu kuwaua watoto wengine sita.
Mashtaka mawili ya kujaribu kuua yanahusiana na mtoto mmoja.
Letby hakupatikana na hatia ya mashitaka mawili ya kujaribu kuua na baraza la majaji halijaamua juu ya mashtaka zaidi ya kujaribu kuua yanayohusiana na watoto wanne.
Leby hakuwepo katika hukumu hiyo na Waziri Mkuu Rishi Sunak alisema serikali inapanga kubadilisha sheria ili kuwalazimisha wafungwa kuhudhuria hukumu.
Mama mmoja aliyefiwa alisema alichukia ukweli kwamba Lucy Leby alikuwa mtu wa mwisho kumshika mtoto wake mchanga
Mwingine alisema: “Sidhani kama tutawahi kushinda ukweli kwamba binti yetu aliteswa hadi hakuwa na vita tena ndani yake.”
Mama wa mtoto wa kike aliyeachwa na ulemavu mkubwa baada ya Leby kujaribu kumuua alisema binti yake “hatawahi kulala, kwenda shule ya upili, kuwa na mchumba, kuolewa”