Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Alexis Sanchez huenda akarejea Inter Milan.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile mwenye umri wa miaka 34 kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Marseille mwishoni mwa msimu uliopita.
Sanchez amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kurejea Barcelona msimu huu wa joto huku miamba hao wa Uhispania wakiendelea kutafuta mikataba ya bei nafuu.
Lakini Mkurugenzi Mtendaji wa Inter, Giuseppe Marotta amependekeza kuwa anaweza kurejea kwa wababe hao wa Serie A, mwaka mmoja baada ya wote kukubaliana kusitisha mkataba wake katika klabu hiyo.
Anadai mchezaji huyo ana nia.
Marotta alisema: “[Joaquin] Correa anataka kuwa na nafasi zaidi na ndio, Sanchez anatamani kurejea hapa.
“Alexis alitutumia ujumbe wazi kuhusu nia yake ya kujiunga tena na Inter, ni kweli.”