Mason Greenwood huenda akapewa ofa ya pauni milioni 10 kwa mwaka ili kujiunga na klabu ya Al-Ettifaq ya Saudi Pro League, kulingana na ripoti.
The Red Devils wamethibitisha Greenwood hana mustakabali wa kuishi Old Trafford baada ya uchunguzi wa ndani uliofuatia kukamatwa kwake Januari 2022.
Kulingana na gazeti la The Sun, kikosi cha Steven Gerrard cha Saudi kina nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye mashtaka yote dhidi yake yalitupiliwa mbali na CPS mapema mwaka huu.
Pia inadaiwa vigogo wa Uturuki Galatasary wameingia kwenye kinyang’anyiro cha Greenwood.
United kwa sasa wanaamua kama kusitisha mkataba wa mshambuliaji huyo na kukubaliana suluhu, au kumwacha apitie soko la uhamisho.
Tazama zaidi…