Mabingwa wa Saudia Pro League Al Ittihad wameanza mazungumzo na Manchester United kujadili kuhusu kumsajili Raphael Varane, ambaye amepewa ‘dalili chanya’ kuhusu uhamisho huo.
Hayo ni kwa mujibu wa ripoti kutoka Saudi Arabia, ambayo inaongeza kuwa mazungumzo yako katika hatua ya awali.
Ilidaiwa wiki iliyopita kwamba Varane, 30, anataka kutumia angalau msimu mmoja zaidi na United kabla ya kufikiria mustakabali wake.
Beki huyo wa zamani wa Real Madrid amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa Mashetani Wekundu na kuhamia Al Ittihad kutamwezesha kuungana na wachezaji wenzake wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Karim Benzema na N’Golo Kante.
tazama zaidi…..