Mkufunzi wa Chelsea Mauricio Pochettino atamkosa moja ya cheche za mafanikio kwenye klabua msimu mpya kutokana na jeraha.
Carney Chukwuemeka amekaa nje kwa wiki sita kutokana na jeraha la goti ambalo ni pigo kubwa kwa meneja wa Chelsea Mauricio Pochettino.
Kiungo huyo mshambulizi anayetegemewa alianza mechi zote mbili za mwanzo za Ligi ya Premia chini ya Pochettino lakini akatoka kwenye kichapo cha 3-1 dhidi ya West Ham.
Chukwuemeka alifanyiwa upasuaji Jumatatu na kuchapishwa kwenye Instagram:
“Kushindwa kidogo lakini nitarejea nikiwa na nguvu zaidi kuliko hapo awali. Asanteni mashabiki wa Chelsea kwa upendo na sapoti yenu. Tutaonana hivi karibuni.”
Taarifa ya Chelsea Jumanne asubuhi.
“Carney Chukwuemeka alipata jeraha kwenye goti lake la kushoto wakati wa mchezo wetu dhidi ya West Ham United Jumapili. Jana usiku Carney alifanyiwa upasuaji na sasa ataanza kupata nafuu.
“Mchezaji huyo wa miaka 19 atafanya kazi na idara ya matibabu ya kilabu katika ukarabati wake huko Cobham.”