Serikali imeanzisha mpango maalum wa kuhakikisha korosho zote zinazovunwa nchini kuhakikisha zinabanguliwa hapa hapa ndani ya nchi badala ya kuuzwa nje.
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa kilimo na mbunge wa dodoma Anthony Mavunde siku ya leo baada ya kufanya ziara ya kukagua utendaji kazi wa viwanda viwili vya korosho kimoja kikiwa na kazi kubangua korosho na kingine ni kukamua mafuta kupitia maganda ya korosho vinavyopatikana wilaya ya mkuranga mkoa wa pwani.
Naibu Waziri Mavunde ameongezea kuwa bajeti ya wizara ya kilimo imepanda kutoka shilingi bilioni 292 mpaka shilingi bilion 970.
Eneo ambalo limeongezewa pesa nyingi ni eneo la ugani na kununua pikipiki kwa maafisa ugani ili wawafikie wakulima kuwahudumia ili walime kilimo cha kisasa ili tuongeze tija kwenye uzalishaji kwasababu wasipolika kwa kisasa hatuwezi ongeza tija kwenye uzalishaji bila hivyo nwatakua wakilima eneo kubwa lakini mavuno machache