Umoja wa Afrika (AU) umeisimamisha Niger kutoka kwa shughuli zake zote kufuatia mapinduzi ya kijeshi mwezi uliopita.
Baraza la Amani na Usalama la AU lilitoa wito kwa nchi zote wanachama wake na jumuiya ya kimataifa kujiepusha na hatua zozote zinazoweza kuhalalisha utawala wa kijeshi nchini Niger.
Ilikariri wito kwa viongozi wa mapinduzi kumwachilia huru Rais mteule Mohamed Bazoum.
Kundi la kanda ya Afrika Magharibi la Ecowas tayari limetishia hatua za kijeshi kumrejesha kazini.
Serikali ya Niger imesema kuwa utawala wa kiraia hauwezi kurejeshwa kwa miaka mitatu, lakini hili limepuuzwa na Ecowas kuwa halikubaliki.