Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa mwanamume mmoja ameagizwa kulipa faini ya shilingi 850,000 ($5,600; £4,400) baada ya kufichua madai ya rafiki yake kuwa na VVU katika kundi la WhatsApp.
Uamuzi huo ulitoka kwa Mahakama ya VVU na Ukimwi nchini Kenya, ambao walisema kwamba hali ya VVU ya mtu haipaswi kufichuliwa kwa wahusika wengine bila idhini.
Mlalamikaji huyo alisema kutokana na ujumbe huo katika kundi la WhatsApp lililokuwa na wanachama 170, alikumbana na ubaguzi na sasa anafanyiwa ushauri nasaha kutokana na matatizo ya kisaikolojia.
Aliongeza kuwa shutuma hizo zimesababisha mtafaruku katika ndoa yake na anakanusha ufichuzi uliotolewa kwenye kundi la WhatsApp.
Pia amepatiwa shilingi 3,000 KE kama fidia maalum