Raia wa Zimbabwe wanapiga kura kuwachagua wabunge na rais katika uchaguzi ambao upinzani unalenga kumaliza utawala wa miaka 43 ya chama tawala wa Zanu-PF.
Hata kabla ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa, misururu mirefu tayari ilikuwa imeanza kuonekana Mbare, kitongoji kidogo kidogo cha mji mkuu Harare.
Baadhi ya wapiga kura waliambia BBC kwamba walikuwa na shauku ya kutekeleza haki zao ya kushiriki uchaguzi.
Uchumi wa nchi hiyo umedorora lakini msemaji wa serikali alisema anaamini raia wa Zimbabwe wanataka kumpa Rais Emmerson Mnangagwa muhula mwingine wa uongozi.
Kipindi cha kampeni kilikabiliwa na kukamatwa kwa wanaharakati wa chama cha upinzani cha Citizens Coalition for Change, ambacho hakijaangaziwa sana kwenye vyombo vya habari vya serikali.
Wapiga kura milioni 6.5 wanatarajiwa kujitokeza kushiriki uchaguzi huo wa leo. Upigaji kura utafungwa saa 19:00 kwa saa za Harare.