Nchini Kenya, watu wawili wameuawa na nyumba nane kuteketezwa moto, likiwemo Kanisa moja, baada ya magaidi wa Al Shabab katika Kaunti ya Lamu, Pwani ya nchi hiyo. hapo jana Jumanne.
Akithibitisha tukio hilo, naibu wa Kamishna kaunti ya Lamu Gabriel Kioni, amesema wanamgambo hao waliwavamia wakaazi eneo la Salama na kuteketeza nyumba nane, pamoja na kutekeleza uharibifu.
‘‘Waliweza kuharibu chakula ambacho kwa sasa hatujui ni kiasi gani lakini pia waliweza kubeba chakula kingine, na vilevile mifugo mbuzi kama saba pamoja na kuuwa mbuzi wengine.’’alisemanaibu wa Kamishna kaunti ya Lamu Gabriel Kioni.
Watu hao wanaodhaniwa kuwa ni magadi kutoka nchi jirani ya Somalia, wamekuwa wakitekeleza mashambulio katika kaunti jirani na Kenya kwa muda sasa.
Kwa sasa idara ya usalama katika kaunti hiyo ya Lamu imewataka raia kuwa waangalifu pamoja na kutoa ushirikiano kwa walinda usalama kwa kutoa habari zitakazowasaidia.