Waziri wa zamani wa mafuta wa Nigeria Diezani Alison-Madueke ameshtakiwa kwa makosa ya utoaji hongo nchini Uingereza.
Anashukiwa kukubali zawadi za kifedha kwa kutoa kandarasi za mamilioni ya dola za mafuta na gesi.
Mhusika mkuu katika utawala wa Rais wa zamani Goodluck Jonathan, pia aliwahi kuwa rais wa kwanza mwanamke wa kundi la
wasafirishaji mafuta la Opec.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 63, ambaye amekuwa kwa dhamana tangu kukamatwa kwake London mwaka 2015,
amekanusha madai ya rushwa.
Mali zenye thamani ya mamilioni ya pauni zinazohusiana na makosa yanayodaiwa zimezuiwa kama sehemu ya uchunguzi
unaoendelea na Shirika la Kitaifa la Uhalifu la Uingereza(NCA).
‘Mashtaka haya ni hatua muhimu katika uchunguzi wa kina na tata wa kimataifa,’ Andy Kelly, kutoka Kitengo cha Kimataifa
cha Ufisadi cha NCA, alisema.
Kwanza alishikilia wadhifa wa waziri wa uchukuzi, kisha akahamia wizara ya madini kabla ya kuchukua nafasi ya
mafuta.
Bi Alison-Madueke, ambaye kwa sasa anaishi katika kitongoji cha St JohnWood, London, atafikishwa katika Mahakama ya
Westminster tarehe 2 Oktoba, NCA inasema.
Nigeria ni mojawapo ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi duniani,ni miongoni mwa wanachama 13 wa shirika la nchi
zinazouza Petroli (Opec), iliyoundwa kushughulikia usambazaji wa mafuta duniani kote