Mwana Diaspora anaejulikana kwa jina la Marycuron kutoka Austria yeye na mume wake kupitia Organisation yao LOVE and CHARITY (Liebe und Hilfeverein Austria) wamejenga na wameifungua leo tarehe 19 .08.2023 shule ya watoto wa chekechea ya kidini hapo Mwanarumango.
Shule hiyo ina madarasa makubwa matatu kwanza watoto wanaoanza, pili watoto wanaojitaharisha kwenda kidato cha kwanza na tatu madrasa ya kidini ambayo jioni inatumika pia na watu wakubwa kujisomea.
Wazo hilo walilipata mwaka 2019 walipotembeliea shule hiyo na kuona watoto wamejazana kwenye darasa moja na wamekaa chini hakuna hata madawati ndipo wakaanza kuwajengea na pia kuwanunulia madawati.
Marycuron ametowa ushauri kwa Wanadiaspora wote kila wanaporudi nyumbani basi watembelee sehemu mbalimbali kusaidia jamii yetu kwa chochote wanachoweza..KUTOA NI UAMUZI SIO UTAJIRI na pia amesisitiza kwa wanadiaspora wote kuacha tabia ya kulaumu kuwa huku nyumbani mambo hayaendi vizuri kama huko ughaibuni bali wajitolea kwa njia yeyote kuboresha na kuleta walichokiona au kukisoma huko huku nyumbani.